Usitishaji mapigano umekaribishwa Sudan Kusini lakini maelfu bado wanahitaji msaada

24 Januari 2014

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yamekaribisha utiaji saini hatua ya kusitisha mapigano baina ya serikali ya Sudan Kusini na majeshi ya waasi , lakini yanasema maelfu ya wakimbizi wa ndani bado wanahitaji haraka msaada wa kibinadamu. Joseph Msami na maelezo zaidi

(RIPOTI YA JOSEPH MSAMI)

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeelezea matumaini kwamba usitishaji mapigano utatekelezwa haraka ili kuepusha wakimbizi wa ndani na nje kuongezeka. Kwa upande wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema machafuko ya karibuni yamekuwa kikwazo kwa maisha ya maeklfu ya Wasudani Kusini watakaohitaji msaada kwa miezi kadhaa ijayo.

Tangu kuzuka kwa machafuko katikati ya Desemba Wasudan Kusini 490,000 wamekuwa wakimbizi wa ndani na wengine zaidi ya 100,000 wamekimbilia nchi jirani za Uganda, Ethiopia, Kenya na Sudan. Kwa mujibu wa Elisabeth Byrs msemaji wa WFP, ugawaji wa chakula kwa wale wanaokihitaji umekuwa ikikabiliwa na uporaji kila wakati.

(SAUTI YA ELISABETH BYRS)

 “Lakini ni muhimu kubaini kwamba mahitaji ya kibinadamu yataendelea baada ya mapigano kusita.Fursa ya kuwafikia walengwa na uporaji wa akiba ya chakula ndio vinavyotia hofu.  Kutokana na uporaji ulioripotiwa kwenye maghala ya WFP , tunakadiria kwamba tumepoteza zaidi ya tani 3700 za chakula ambazo zinatosha kulisha watu zaidi ya 220,000 kwa mwezi mmoja. Tunafanya tuwezalo kulinda akiba zingine za chakula ambazo kinaweza kuporwa.Ghala la WFP Malakal limesalia tupu baada ya matukio ya kila mara ya uporaji