Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunajitahidi kuongeza operesheni zetu pale panapowezekana:WFP

Tunajitahidi kuongeza operesheni zetu pale panapowezekana:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanza operesheni kubwa ya dharura ili kuwafikishia chakula maelfu ya watu wanaokimbia mapigano katika taifa jipya kabisa la Sudan Kusini.

Ukosefu wa usalama unamaanisha kwamba kuwafikishia chakula wmaelfu ya watu wenye njaa ni changamoto, lakini hata hivyo tangu kuzuka kwa machafuko WFP imeweza kuwafikia watu 178,000 wanaohitaji msaada. Kwa mujibu wa Challiss McDonough wa WFP sehemu kubwa ya mji wa Bor umeharibiwa vibaya na mapigano yaliyosambaratisha Sudan Kusini, mitaa imesalia tupu huku idadi kubwa ya wakazi wamefunga virago na kukimbilia kusalimisha maisha yao.

Lakini hata pale ambapo miji imetelekezwa WFP imejitahidi kuingia na kugawa chakula, na sasa imemaliza kugawa kwa watu 9,000 walioamua kubaki na kutafuta hifadhi kwenye ofisi za Umoja wa mataifa. Miji mingine kama Bentiu na Malakal ni kama Bor mapigano yamekuwa makali kwa muda.

Hata hivyo WFP inasema vitendo vya uporaji ni tatizo kubwa na wanahofia tani 4000 za chqakula zimeporwa kwenye ghala lake. Mbali ya Sudan Kusini WFP inatoa msaada kwa wakimbizi 86,000 waliovuka mpaka na kuingia nchi jirani za Uganda,Ethiopia,Sudan na Kenya.