Tume ya fidia ya UM yalipa dola bilioni 1.3

23 Januari 2014

Tume ya fidia ya Umoja wa Mataifa Alhamisi imelipa dola bilioni 1.03 kwa serikali yaKuwaitikiwa ni deni lililosalia kwa nchi hiyo kwa ajili ya kuwalipa waathirika fidia.

Tume ya fidia ya Umoja wa Mataifa ilianzishwa mwaka 1991 kufuatia azimio la baraza la usalama namba 687 na 692 lililotaka kushughulikiwa kwa madai na kulipa fidia kwa hasara na uharibifu kwa watu binafsi, mashirika, serikali na mashirika ya kimataifa kutokana na uvamizi wa Iraq huko Kuwait kuanzia tarehe pili Agosti mwaka 1990 hadi tarehe pili Machi mwaka 1991.

Tume hiyo ilipokea mdai karibu milioni 2.7 na ikakamilisha kuyatathimini yote mwaka 2005. Na takribani dola bilioni 52.4 zimelipwakamafidia kwa serikali zaidi ya serikali na mashirika ya kimataifa 100 ili zigawanywe kwa madai milioni 1.5.

Madai yanayopitishwa yanalipwa na mfuko wa fidia wa Umoja wa mataifa unaopokea fedha asilimia 5 zitokanazo na mauazo ya petrol yaIraqna bidhaa zingine za mafuta.

Kwa malipo ya leo tume hiyo ya fidia itakuwa imeshalipa jumla ya dola bilioni 44.5 huku ikisaliwa na deni la dola bilioni 7.8 pekee za kulipa.