Harakati za UNICEF kukabili utapiamlo Sudan zaungwa mkono

22 Januari 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF litapokoea Euro Milioni Mbili kutoka Ofisi ya usaidizi wa kibinadamu ya Tume ya  Ulaya kwa lengo la kuimarisha harakati za kupambana na utapiamlo nchiniSudan.

Mwakilishi wa UNICEF huko Sudan Geert Cappelaere amesema uhai wa mtoto nchini humo unakabiliwa na vitisho kadhaa ikiwemo utapiamlo na kwamba watoto wapatao Laki Saba na Nusu wenye umri wa chini ya miaka mitano wanahitaji tiba kutokana na utapiamlo uliokithiri.

Amesema kuwafikia watoto hao ni muhimu kwa mustakhbali wao kiutu na kimaendeleo kwani kuchukua hatua mapema kutaokoa siyo tu maisha yao bali ukosefu wa makuzi yenye afya ambayo ni muhimu kwa maisha yao ya baadaye.

Mwakilishi huyo ameshukuru msaada wa tume hiyo akisema fedha hizo zitatumika kwenye mradi wa kuokoa maisha ya mtoto katika majimbo nane  yaSudanikiwemoDarfur. Lengo ni kufikia watoto Elfu 98 walio na umri wa chini  ya miaka mitano ambapo mradi utajenga uwezo kwa serikali za mitaa na jamii kuwapatia watoto huduma bora za lishe.