Mabadiliko ya hali ya hewa ni ajenda kuu kwenye kongamano la dunia la uchumi Davos:

22 Januari 2014

Mabadiliko ya hali ya hewa yamepangwa kuwa ajenda kuu katika kongamano la kimataifa la uchumi linaloendelea huko Uswizi.

Zaidi ya viongozi 2500 kutoka nchi takriban 100 wakiwemo wakuu wa nchi  na serikali zaidi ya 30 wanatarajiwa kushiriki kwenye siku nne za kongamano la kimataifa la uchumi mjini Davos.

Wawakilishi wa kutoka sekta za umma, binafsi na jumuiya za kijamii wataweka mawazoyaopamoja ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na kubainisha fursa za kiuchumi kwa kuchukua hatua.

Januari 22 imechaguliwa kama siku ya mabadiliko ya hali ya hewa , ili kutanabaisha mchakato unaoendelea mwaka 2014 kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na ajenda ya maendeleo endelevu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon anatarajiwa kuzungumza kuhusu serikali na makampuni ya biashara yatakavyoweza kufanya kazi pamoja kuhusu suala hili.