Wakuu wa mashirika ya misaada ya UM watoa wito wa kuwalinda watoto Syria

22 Januari 2014

Viongozi wa mashirika ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa mataifa na askofu mkuu Desmond Tutu wametoa wito kwa pande zote nchini Syria zinazokutana Switzerland kuchukua hatua ya haraka kuwalinda watoto nchini Syria.

Katika baruayaoiliyoandikwa kabla ya mkutano ulianza leo Jumatano, Montreux  wakisema zaidi ya watoto 11,000 wa Kisyria wameshapoteza maisha yao.

Kuanzia makombora yanayovurumishwa kwenye makazi ya watu hadi mashambulizi mashuleni na hospitali , watoto wamekuwa wakilengwa imesema barua hiyo”

Wakuu wa mashirika ya Umoja wa mataifa pia wamesema zaidi ya watoto milioni nne wamekimbia nyumba zao wakiwemo zaidi ya milioni moja waliokimbilia nchi jirani.

Wakuu hao wameongeza kuwa watoto wengi wameathirika , wananjaa na wanahitaji malazi na ulinzi. Na cha kashifa zaidi misaada haiwezi kuwafikia watoto wanaoihitaji zaidi.

Viongozi hao pamoja na Askofu mkuu Desmond Tutu wamewataka washiriki katika mkutano wa Syria kutowalenga watoto na kujikita katika mpango wa kuwalinda.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter