Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tamko la Geneva ndio msingi wa hatma ya Syria; Marekani, Urusi

Tamko la Geneva ndio msingi wa hatma ya Syria; Marekani, Urusi

Marekani na Urusi ambazo zimekuwa mstari wa mbele kufanikisha mkutano wa kimataifa wa amani kuhusu Syria, zimesema mashauriano ya Montreux nchini Uswisi yaliyotangulia mkutano huo utakaofanyika Ijumaa, ni fursa pekee ya kuleta amani ya kudumu.

Wajumbe wa pande hizo wakizungumza wakati wa ufunguzi wa mashauriano hayo yaliyolenga kuonyesha mshikamano na Syria wamesema wakati ni huu na tamko la pamoja laGenevala tarehe 30 Juni 2012 ndio dira ya hatma ya Syria.

Tamko hilo pamoja na mambo mengine linataka kuundwa kwa maridhiano ya pande husika, serikali ya mpito yenye mamlaka kamili. Marekani iliwakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje John Kerry, yeye alisema ni wakati wa kukabiliana na hali halisi.

(Sauti ya Kerry)

 “Sasa  tunahitaji kukabiliana na hali halisi. Bila shaka tunahitaji kuangalia hali halisi. Maridhiano ya pamoja yaliyotuleta hapa kwa ajili ya serikali ya mpito, serikali ya mpito ambayo haiwezi kuundwa na mtu ambaye anakubaliwa na  upande mmoja au mwingine.”

 

Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi aliiwakilisha nchi yake kwenye mazungumzo yake akisema kuwa jukumu la pamoja na kumaliza madhila yanayokumba wananchi waSyria. Amesisitiza kuwa suluhu la mzozo waSyriani kupitia mazungumzo baina ya pande zinazohusika  nchini humo na bila matumizi ya nguvu za kijeshi.

Bwana Lavrov amesema wanapoanza mashauriano baina ya pande husika nchiniSyriawanazisihi pia kujadili hatmayaokwa kuzingatia tamko la Genevana azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huku akisisitiza kuwa msingi wa tamko la Geneva ni pande husika kuwa na maafikiano bila shinikizo kutoka upande wowote.