UM waongeza misaada kuwafikia manusura wa mapigano Iraq

21 Januari 2014

Kufuatia kuongezeka kwa idadi ya watu waliopoteza makazi na familia kadhaa kushikiliwa kutokana na mapigano yanayoendelea katika miji tofauti jimboni Anbar nchini Iraq Umoja wa Mataifa umeongeza misaada ya kiutu ili kuzinusuru jamii hizo.

Mathalani hadi January 20 zaidi ya familia 22,000 zimejiandikisha kama wakimbizi wa ndani wengi wao wakiwa jimboni Anbar na maeneo mengine kama Erbil, Salah-Al-Din, Kerbala, Babylon, Najaf, na Baghdad.

Hata hivyo idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi kwani sio wote ambao wamepoteza makazi yao wamejiandikisha. Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Nickloay Mledanov amesema ofisi yake itandelea kufanyakazi kwa karibu na serikali ya Iraq, jimbo la Anbar viongozi wa kijamii ili kuzifikia familia katika maeoneo ambapo mapigano yanaendelea pamoja na wale wanaokimbia mapigano hayo.