Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu muhimu wa UM wataka mkutano wa Geneva II kufikia muafaka wa amani:

Wataalamu muhimu wa UM wataka mkutano wa Geneva II kufikia muafaka wa amani:

Kundi la wawakilishi ambao ni wataalamu wa masuala ya haki za binadamu kwenye mfumo wa Umoja wa mataifa wametoa wito kwa mkutano ujao wa Syria, Geneva II kuafikiana kuhusu hatua za kumaliza machafuko kwa amani.

Katika barua yao ya wazi iliyochapishwa leo Jumanne wataalamu hao pia wametaka kuwe na lengo na wajibu wa amani ya kudumu ambayo italinda haki za binadamu wote.

Kwa mujibu wa Chaloka Beyani aliyezungumza kwa niaba ya kamati inayoratibu kazi za wataalamu hao maalumu , maisha, hatma na haki za msingi za mamilioni ya raia walioathirika yako katika hatihati nchini Syria.