Ndege ya kwanza ya UNICEF yawasili Juba kunusuru afya za wanawake na watoto.

21 Januari 2014

Ndege ndogo ya kwanza miongoni mwa ndege mbili za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, ikiwa na tani 35 za misaada ya dharura nchini Sudan Kusini zimewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba . Grace Kaneiya na maelezo zaidi

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Ndege hiyo imebeba vifaa vya tiba kwa ajili magonjwa mbalimbali ikiwamo malaria , vichomi vikali yaani pneumonia , kuharisha na utapiamlo pamoja na virutubisho na vitamini, antibiotics na dawa za kupunguza maumivu.

Misaada hii inayotarajiwa kuleta hueni kubwa kwa wanawake na watoto wanaokumbwa na madhila ya vita pia inahusiha wakunga wa jadi na vifaa vya upasuaji kwa ajaili ya uzazi na vifaa vitakavyosadia kutoa huduam ya maji safi na usafi kw aujumla. Dermot Carty ni Mkurugenzi wa operesheni wa UNICEF Sudani Kusini

(SAUTI YA DEMOT CARTY)

"Kwa sasa kama unavyofahamu maeneo yahafikiki kutokana na usalama na tunajaribu kudadilisha mipango yetu ili tunyumbulike na kutumia fursa tayari kutoa misaada. Tunaandaa timu tayari kwenda kuyafiki maeneo lakini hili linategema hali ya usalama. Ndege ya pili inatarajiwa kuwasili alhamaisi nah ii inategemea idadi ya watu waliopoteza makazi na wanaohitaji misaada tutahitaji kutoa misaada zaidi."