Plumbly alaani shambulio la bomu kusini mwa Beirut

21 Januari 2014

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, Derek Plumbly, amelaani vikali shambulizi la bomu lililochukuliwa kwa gari leo asubuhi kwenye mtaa wa makazi na biashara wa Haret Hreik kusini mwa Beirut, na ambalo limewaua watu kadhaa na na kuwajeruhi wengine.

Ametuma risala za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulio hilo

Plumbly amesema, shambulio la leo, ambalo ni la tatu katika kipindi cha wiki tatu, ni tukio jingine linalodhihirisha ugaidi usiobagua walengwa. Amesema vitendo kama hivyo haviwezi kukubaliwa, na ni kinyume na matakwa ya watu wa Lebanon wote.

Ametowa wito kwa watu wa Lebanon waungane, na kuchukua hatua zote zinazoweza kuimarisha umoja wa kitaifa, ikiwemo kasi ya hivi karibuni ya kuunda serikali mpya.