Kay apongeza kuundwa baraza kuu la utawala wa Juba

20 Januari 2014

Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, balozi Nicholas Kay amekaribisha kuanzishwa kwa baraza kuu la utawala wa mpito wa Juba ambapo Sheikh Ahmed Madobe Islan ameteuliwa kuwa kiongozi wake

Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa baraza hilo mjini Kismayo Kay pia amepongeza kuteuliwa kwa mawaziri na kaimu kiongozi wa baraza hilo, aikieleza matumaini yake kuwa utawala huo ni hatua muhimu katika mchakato wa kutekeleza makubaliano ya August 27 ya Addis Ababa.

Ametaka makabidhiano ya uwanja wa ndege wa Kismayo na bandari, kurejeshwa na kuungamanishwa na jamii kwa wanamgambo kutekelezwa kama jambo la dharura.

Kadhalika balozi Kay amerejelea hakikisho la ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM, la kuendelea kufanya kazi na wabia wa kimataifa kuunganisha rasilimali katika kusadia utawala huo kwa kuwezesha mijadala, kutoa msaada wa kitaalamu na kusaidia serikali katika muundo wa taifa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter