Kiwango cha ukuaji uchumi kuongezeka 2014-2015 ikilinganishwa na 2013

20 Januari 2014

Ripoti mpya kuhusu hali ya uchumi duniani na matarajio ya ustawi kwa mwaka 2014 imeonyesha matarajio ya kukua kwa uchumi kwa mwaka huu na ujao licha ya kiwango cha chini cha ukuaji mwaka jana. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Ripoti ya Assumpta)

Ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2013 ulikumbwa na misukosuko licha matumaini hapo awali, imesema ripoti hiyo ikitaja kuwa kiwango cha ukuaji kilifikia asilimia 2.1  na sababu ni nchi tajiri kuendelea kung’ang’ana kuhimili changamoto zilizotokana na mdororo wa kiuchumi huku zile zinazoibukia nazo zikipata fursa nzuri za ndani na za nje baada ya misukosuko ya kipindi cha miaka miwili.Nchi hizo zinazoibukia ni pamoja na China,  India na Brazil. Ripoti inasema mwaka 2014 kiwango cha ukuaji kitakuwa asilimia 3.0 ilihali 2015 asilimia 3.3.

Hata hivyo licha ya matumaini hayo, ukosefu wa ajira kwenye nchi tajiri na maskini umetajwa kuwa changamoto kubwa na hivyo sera madhubuti zinahitajika ili kuondoa hali hiyo hususan miongoni mwa vijana.