Athari za kimbunga Haiyan zachagiza maandalizi ya mapema ya msimu wa vimbunga:

20 Januari 2014

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza athari za majanga UNISDR, limeungana na sekta ya kimataifa ya bima kupendekeza mtazamo mpya na mkubwa wa kufadhili athari za majanga kwa Ufilipino mapema wakati msimu wa typhoon ukijongea mwaka huu ,wakati ambapo taifa hilo bado linakabiliana na hasara ya dola bilioni 13 zilizosababishwa na kimbunga Haiyan/ Yolanda.

Mkuu wa UNISDR, Margareta Wahlström, amesema leo kwamba Ufilipino inakumbwa na tufani zaidi ya 20 kila mwaka na kinachohitajika ni utaratibu rahisi ambao utatoa ulinzi wa bima kwa watu na miji yao kabla ya msimu mwingine wa vimbunga.

Ameongeza kuwa na ili mfumo huo uwe na mafanikio basi utahitaji kutekelezwa kwa lazima na vitengo vya serikali katika maeneoyao, lakini itawafanya kudhibiti mustakhbali wao, hasa inapokuja hali ya kukabiliana na mahitaji na ujenzi mpya kunapotokea janga kubwa.

Mradi wa bima ya majanga ulioanzishwa na wadau wakubwa wa kimataifa wa masyuala ya bima.