CAR iko hatarini kutumbukia kwenye machafuko ya kidini: Pillay

20 Januari 2014

Ofisi ya Kamishna ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imetaka kuchukuliwa hatua za haraka ili kuzuia uwekekano wa kujitokeza zaidi kwa machafuko ya kikabila katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. George Njogopa na taarifa kamili

 (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kamishna Mkuu wa Ofisi hiyo Navi Pillay amesema kuwa kukosekana kwa dola yenye idhini pamoja na kuendelea kutoheshimiwa kwa haki za binadamu ni mambo ambayo yanazidisha hali ya shaka kuhusu majaliwa ya taifahilo.

Akizungumza wakati wa kikao maalum cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo linakutana kwa dharura kwa ajili ya kujadilia hali ya mambo katika Jamhuri ya Kati, Bi Pillay amesema kuwa kuna haja ya kuchukuliwa hatua za haraka kudhibiti ukorofi unaoendelea.

Amesema pande zote kuanzia jumuiya za kimataifa, wanasiasa wa ndani, taasisi za kidini pamoja na mashirika ya kiraia zinawajibu wa kuhakikisha kwamba mapigano yanayoendelea yanasimama.

Ameleeza kuwa wachunguzi wa haki za binadamu wamebaini kuwepo kwa vifo zaidi ya 1,000 vilivyotokea katika mji mkuu waBanguikwa kipindi cha disemba 5 na 6 mwaka uliopita

 (SAUTI YA NAVI PILLAY)

"Ujumbe ulikusanya maelezo mengine yanayoonyesha kuwepo kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo vile vya unyanyasaji wa kijinsia, watu kulazimishwa kuondoka kwenye maeneo yao mateso na matukio mengine ya utesaji mkubwa.Pia kulikuwa na matukio ya utiaji mbaroni watu ovyo na wengine kushukiliwa kwa nguvu, na kuchomwa moto kwa makanisa na misikiti."

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka hatua za makusudi za kumaliza kile kinachoendelea nchini  humo kwani mvutano wa kidini kamwe haujawahi kuwa chanzo cha mzozo Jamhuriya Afrika ya Kati.