Kongamano la wiki ijayo ni muhimu katika kutafuta suluhu kwa mzozo Syria:Ban

17 Januari 2014

Kongamano la kimataifa kuhusu harakati za amani nchini Syria, linatazamiwa kuanza wiki ijayo mnamo tarehe 20 Januari. Kongamano hilo ambalo kuwepo kwake kumekumbana na changamoto nyingi, linatarajiwa kutoa nafasi muhimu ya kupata suluhu la kisiasa kwa mzozo wa Syria, ambao umekuwa ukitokota kwa miaka mitatu sasa.

Baada ya muda mrefu wa kujaribu kuzishawishi pande zinazozozana kuelekea kwenye meza ya mazungumzo, maandalizi ya kongamanohiloyamepata pigo wiki hii, baada ya kundi moja muhimu miongoni mwa wahusika watarajiwa kutangaza kuwa halitoshiriki mazungumzo hayo.

Basi wakati tarehe hiyo ikikaribia, ungana na Joshua Mmali, akiangazia hapa hali ilivyo na maandalizi yanayofanywa kabla ya kongamano hilo.

(Makala)