Zana za kilimo zaleta mapinduzi ya kilimo duniani.

17 Januari 2014

 Zana za kisasa za kilimo zimehuisha kilimo husuani barani Afrika na hivyo kupunguza adha za mamilioni ya familia za wakulima duniani  barani humo limesema shirika la chakula na kilimo FAO.

Kwa mujibu wa chapisho la FAO lenye jina zana za kilimo kwa ajili maendeleo vijiini, mapitio ya mifumo na maendeleo duniani, ukuaji usiokwepeka wa matumizi ya pembejeo unatoa funzo kwa watunga sera na wachumi kutoka maeneo yaliyopiga hatua katika kilimo na ukanda uliokuwa nyuma.

 Chapisho hilo linataja nchi ambazo zilikuwa nyuma katika kilimo cha zana za kisasa kama Bangladesh, nchi za Asia Kusini na Afrika ambapo inaelezwa kuwa inaongoza kwa kuwa na ardhi iliyotelekezwa huku takwimu zikionyesha kwamba asilimia 60 ya nguvu kazi ya kilimo hutegemea wanawake,wazee na watoto lakini sasa zana hizi zimeleta mapinduzi.

 Kwa mujibu wa Mkurugenzi Msadizi wa idara ya kilimo na ulinzi wa walaji ndani ya FAO Ren Wang chapisho hilo sio tu linaeleza namana zana hizi zitachangia katika maendeleo endelevu ya mazingira bali pia namna sera zitakvyoweka umuhimu wa zana za kilimo  kwa famili za wakulima ili wanufaike.

 Mapinduzi haya yanatajwa kuwa zana muhimu pia katika mapambano dhidi ya umasikini.