Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gharama kubwa ya mishahara ya watumishi serikalini Zambia yatishia uchumi: IMF

Gharama kubwa ya mishahara ya watumishi serikalini Zambia yatishia uchumi: IMF

Shirika la fedha duniani, IMF limesema mafanikio ya kiuchumi yaliyokuwepo nchini Zambia yanakabiliwa na changamoto kubwa ya nakisi ya fedha.

Mkuu wa IFM nchini humo John Wakeman-Linn amesema serikali ya Zambia inatumia fedha nyingi zaidi kuliko inazokusanya kwenye kodi na hivyo kutishia uchumi. Mathalani ametaja gharama ya mishahara kwa watumishi wa serikali ambayo ni asilimia 54 ya mapato ya serikali.

Amesema hali hiyho si endelevu kwa hiyo ni lazima kupunguza nakisi hiyo sasa ili kupunguza athari kwa soko la fedha na hata kwa wawekezaji.

(Sauti ya Wakeman-Linn)

 

Kudhibiti gharama za mishahara kwa wafanyakazi ni muhimu iwapo serikali ya Zambia inataka kuchukua hatua kwa nakisi ya fedha. Kiwango cha gharama za mishahara Zambia iwe ni kwa upande wa mapato au kwenye GDP ni miongoni mwa viwango vikubwa zaidi au pengine ni kikubwa zaidi kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Serikali ilitambua hilo na hivyo kwenye bajeti imependekeza kusitisha nyongeza ya mishahara mwaka 2014.2015 na pia kusitisha ajira mpya mwaka 2014,. Na hiyo ni hatua nzuri na kweli ni muhimu kama hatua za awali za kudhibiti bajeti ya mishahara.”

 Kwa muongo mmoja uliopita, kiwango cha ukuaji uchumi nchini Zambia kilikuwa ni kati ya asilimia Sita hadi Saba na kwa mujibu wa IMF hiyo inatokana na sera thabiti za uchumi na bei thabiti ya madini yaShaba.