Utawala wa Sheria waweza kuwa kichochezi cha fursa jumuishi za maendeleo: Eliasson

17 Januari 2014

Hii leo kwenye Umoja wa Mataifa, umefanyika mdahalo kuhusu utawala wa sheria na jinsi unavyoweza kuwa kichochezi cha fursa jumuishi za maendeleo. Mdahalo huo umefanyika kabla ya mazungumzo ya kamati ya kuchukua hatua kuhusu malengo ya maendeleo endelevu.

Mdahalo huo umefanyika ili kuangalia jinsi ujumuishaji wa suala la utawala wa sheria katika ajenda ya maendeleo unaweza kuchangia kwa njia muhimu kwenye mkondo wa maendeleo yenye usawa na endelevu, na hivyo kunufaisha serikali, jamii na watu binafsi. Akizungumza wakati wa mjadala huo, Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson amesema…………

(SAUTI YA ELIASSON)

“Uongozi wa kisheria unaweza kuhakikisha uwajibikaji na kusaidia huduma za msingi kama vile elimu, afya na majisafi kupatikana kwa watu wote. Uongozi wa kisheria unawawezesha wananchi kushughulikia visababishi vya ukosefu wa usawa na kuenguliwa kama ilivyobainishwa na malengo ya milenia. uongozi wa kisheria pia ni kigingi cha ufisadi. Ufisadi  unaharibu masoko, unaondoa imani kwa serikali na kukwamisha maendeleo endelevu.”

Mdahalo huo umeandaliwa na Shirika la Kimataifa la Sheria kuhusu Maendeleo, IDLO na idara ya utawala wa sheria katika ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, zikisaidiwa na serikali yaFinland