Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lataka masuala muhimu ya mzozo wa Mali yashughulikiwe

Baraza la Usalama lataka masuala muhimu ya mzozo wa Mali yashughulikiwe

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Wanachama wa Baraza la Usalama wamekaribisha kufanyika kwa uchaguzi wa urais na ubunge hivi karibuni nchini Mali, kama hatua muhimu ya kurejesha uongozi wa kikatiba nchini humo.

Wanachama hao ambao wamesikiliza ripoti ya Katibu Mkuu ilowasilishwa na Mwakilishi wake nchini Mali, Albert Koenders, wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza harakati jumuishi za kisiasa, ambazo zitaleta maridhiano na kukabiliana na masuala muhimu yanayozozaniwa, bila mashartti. Baadaye, rais wa Baraza hilo, ambaye ni mwakilishi wa Jordan, amesoma taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kilichojadiliwa.

“Wameelezea masikitiko yao kuhusu matukio ya ghasia na ugaidi hivi karibuni kaskazini mwa nchi hiyo, na kuhusu na kuelezea umuhimu wa kupinga vitendo kama hivyo na kutoa uungaji mkono unaofaa wa kiusalama, kiuchumi na kijamii, ili kuzuia kuibuka tena kwa makundi ya kigaidi na vitendo vyao.”

Wamesisitiza pia umuhimu wa kuviwezesha vikosi vya ujumbe wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA, kuetekeleza majukumu yake kikamilifu katika nafasi zake zote, zikiwemo polisi, wanajeshi na wahudumu wa kiraia.