Mtaalamu maalum wa UM kuhusu haki za mjumuiko wa amani kuzuru Rwanda.

16 Januari 2014

Maina Kiai, mtaalam maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kujumuika kwa amani atakuwa na ziara rasmi nchini Rwanda kuanzia tarehe 20 mwezi huu.

Hii ni ziara ya kwanza ya Bwana Kiai nchiniRwandaakiwa mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ambapo amesema haki za uhuru wa kujumuika ni misingi ya demokrasia na kwamba baraza la haki za binadamu linataka serikali kuheshimu na kuzilinda.

Amesema ushirikiano wa serikali katika kusimamia haki hizo ni muhimu katika kumwezesha yeye kutekeleza majukumu yake kwa njia yenye ufanisi.

Wakati wa ziara hiyo ya siku nane nchini Rwanda,  Kiai atakutana na viongozi waandamizi wa serikali wakiwemo wale wa mahakama, wawakilishi wa tume ya taifa ya haki za binadamu, taasisi za kiraia na wanadiplomasia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter