UNHCR yalemewa na wingi wa wakimbizi wa Sudani Kusini wanaomiminika Uganda

16 Januari 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), na wadau wake nchini Uganda,  wanakumbana na changamoto mbalimbali kufuatia  kumiminika kwa wakimbizi kutoka Sudan Kusini.Ripoti ya hivi punde inasema, angalau wakimbizi elfu moja wanaingia nchini Humo kila siku. John Kibego wa radio washirika  Spice FM,Ugandana maelezo kamili

 (Tarifa ya John Kibego)

Idadi ya wakimbizi hapaUgandaimefikia 45,000 tangu mapigano ambayo yameingia mwezi wa pili yazuke Sudan Kusini.

Wengi wamesajiliwa katika kambi ya wakimbizi Agago katika wilayai ya mpakani ya Adjumani. Wengine wako katika kambi ya Kiryandongo wilayani Kieyandongo na wengine katika kambi ya Rhino wilayani Arua.

Duru kutoka wanausalama zinasema, kuna karibu wakimbizi 30,000 kwenye eneo la mpakani wakingojea kuvuka waigieUganda.

Lucy Beck msemaji wa UNHCR amedokezea kuwa, kufikia mahitaji yaoya  dharurakamamaji na malazi kwao, bado ni changamoto kubwa.

(Sauti ya Lucy Beck)

”Changamoto kubwa kubwa tunaazo ususani katika utoaji maji na chakula. WFP linajaribu kutoa chakula na kuunda majokoni zaidi. Baado tuna idaadi kubwa ya  wanaolala chini ya miti”

Wafanyakazi zaidi wa kushughulikia wakimbizi hao tayrai wamewasili katika maeneo ya mpakani huko wengine wakiwa safarini, kulingana na UNHCR