Chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu walaani mauaji ya mtu wao Syria

16 Januari 2014

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu wamekasirishwa na kifo cha mfanyakazi wa kujitolea wa shirika la mwezi mwekundu la Syria bwana Hekmat Mohamad Kerbaj, katika tawi lake la Dumair nje kidogo ya mji mkuu Damascus. Mfanyakazi huyo alifariki dunia tarehe 8 Januari baada ya mateso ya miezi 5 aliyokuwa ametoweka waka.

 Bwana Mohamed alikutwa kando ya barabara kwenye eneo la Jaramana, kwenye viunga vya Damascus tarehe 5 ya mwezi huu na akapelekwa hospital lakini hali yake ilikuwa mbaya saana. Kwa jumla wafanyakazi wa kujitolea 34 wa shirika la mwezi mwekundu wamepoteza maisha yao tangu kuanza kwa machafuko nchini Syria .

Na waliuawa baada ya kukamatwa au kutimiza majukumu yao ya huduma za kibinadamu.

Na wakati hali ya kibinadamu ikizidi kuzorota shirika la mwezi mwekundu linasema kifo cha Hekmat kinadhihirisha ugumu na hatari zinazowakabili wafanyakazi wa misaada na wale wanaojitolea nchini Syria.