Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na idadi ya vifo inayoongezeka Sudan Kusini

Ban asikitishwa na idadi ya vifo inayoongezeka Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kuendelea kuongezeka idadi ya watu wanaopoteza maisha nchini Sudan Kusini siyo jambo la kufumbiwa macho.

Amesema kuwa taarifa za watu kuendelea kupoteza maisha ikiwemo na wale 200 walioaga dunia baada ya mashuayaokuzama maji, ni taarifa zinazosikitisha na hivyo pande zinazozozana ziwajibike kuwalinda raia.

Amelaani pia matukio ya kushambulia misafara ya mashirika ya utoaji misaada ya usamaria mwema akisema kuwa vitendokamahivyo havivumiliki.

Amerejelea wito wake akisema kuwa wale wote wanashambulia raia pamoja na watumishi wa Umoja wa Mataifa watapaswa kuwajibika.