Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matukio ya uharamia baharini yapungua

Matukio ya uharamia baharini yapungua

Kiwango cha vitendo vya uharamia baharini kimepungua na kufikia kiwango cha chini zaidi duniani ndani ya miaka Sita na hiyo imeripotiwa kuchochewa na harakati za kudhibiti vitendo hivyo. Ofisi ya kimataifa dhidi ya uharamia na ile ya biashara zinasema mwaka jana pekee kulikuwa na matukio 264 duniani, ikiwa ni pungufu kwa asilimia 40 tangu uharamia huko Somalia ufike kiwango cha juu mwaka 2011. George Njogopa na taarifa kamili

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Katika kipindi cha mwaka 2013, matukio ya uharamia yaliyoripotiwa kutokea katika pwani yaSomaliayalifikia 15, idadi ambayo ni ya chini ikilinganishwa na ile ya mwaka 2012 kulikojitokeza matukio 75.

Katika mwaka 2011 kiwango cha matukio kilikuwa cha hali ya juu, kukiripotiwa matukio 237.

Kulingana na ripoti hiyo ya wakala wa kimataifa, watu 300 walitekwa nyara mwaka uliopita, huku wengine 21 wakijeruhiwa na maharamia hao katika maeneo ya bahari.

Jumla ya vyombo vya majini vilivyotekwa nyara vilifikia 12 huku pia kukiarifiwa kuwepo kwa matukio ya ukatilii kutoka kwa maharamia wenye asili yaNigeria