Japan kuipa msaada Sudan Kusini wa dolla milioni 25

15 Januari 2014

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema nchi yake inajiandaa kutoa msaada wa haraka wa dola takribani milioni 25 kwa Sudan Kusini kukabiliana na hali ya kibinadamu inayozidi kuzorota.

Abe akizungumza wakati wa ziara yake nchini Ethiopia baada ya kutoka Ivory Coast na Msumbiji amesema dola milioni 20 kati ya milioni 25 wanazotoa zitatumika katika katika ombi la haraka lililotolewa na Umoja wa mataifa mwezi Desemba ambapo zitashughulikia mahitaji ya kibinadamu kama chakula na lishe, afya, maji na usafi, misaada ya kiufundi na wakimbizi.

Japan inaunga mkono juhudi zinazofanywa na mataifa mengine na mashirikakamaIGAD katika kutafuta suluhu kwa njia ya amani ya mgogoro wa Sudan Kusini na imetoa wito kwa pande zote nchini humo kuitikia wito wa juhudi za kuleta amani.