Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa nchi zinazoendelea wahitaji vichocheo ili uzidi kuimarika: Benki ya dunia

Uchumi wa nchi zinazoendelea wahitaji vichocheo ili uzidi kuimarika: Benki ya dunia

Miaka mitano baada ya mdororo wa uchumi, Benki ya dunia inasema kuwa kuna viashiria dhahiri kwa uchumi wa dunia kuanza kurejea hali ya kawaida huku nchi zinazoendelea nazo zikimulikwa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Ripoti ya hivi karibuni zaidi ya Benki hiyo kuhusu matarajio ya uchumi wa dunia inaweka bayana kuwa mwelekeo huo chanya unatokana na kuanza kuimarika kwa uchumi wa nchi zenye vipato vya juu jambo linalochochea pia ukuaji kwenye nchi zinazoendelea.

Ripoti inatabiri ukuaji uchumi katika nchi hizo zinazoendelea kuongezeka kutoka asilimia 4.8 mwaka jana hadi asilimia 5.7 mwaka huu. Eneo la Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara uchumi wake uliongezeka ukichochewa na uwekezaji katika sekta ya rasilimali. Andrew Burns ni mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo.

(Sauti ya Burns)

Kiwango cha ukuaji uchumi katika nchi zinazoendelea baada ya mdororo wa uchumi kilikuwa karibu asilimia Mbili zaidi kuliko miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90. Ili kusonga mbele vizuri, kwahitajika kuangalia sera za marekebisho ya muundo kama vile uwekezaji kwenye elimu, miundombini na afya pamoja na sheria nzuri za kuimarisha fursa za ukuaji uchumi kwa nchi husika.”