Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya milioni 3 wafaidika na msaada wa chakula wa WFP Syria:

Watu zaidi ya milioni 3 wafaidika na msaada wa chakula wa WFP Syria:

Shirika la mpango wa chakula lduniani WFP limegawanya msaada wa chakula kwa watu miliioni 3.8 kwa mwezi wa Desemba na kuweka rekodi ya kipekee.

Sasa shirika hilo linaendelea kuimarisha operesheni zake za kiufundi ili kulisha watu milioni Saba mwezi huu wa Januari.Idadi hiyo inajumuisha watu milioni 4.25 walio ndani yaSyriana zaidi ya milioni 2.9 waliopata ukimbizi katika mataifa jirani. Elisabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

 (SAUTI YA ELISABETH BYRS)

 “WFP sasa inahitaji dola Milioni 35 kila wiki kwa ajili ya kusaidia wahanga wa mzozo unaoendelea Syria ambao wanaishi ndani ya nchi yao au nchi jirani.”

Kwa mantiki hiyo WFP itahitaji takribani dola Bilioni Mbili kwa usaidizi wa chakula kwa watu Milioni Saba Mwaka huu wa 2014.