Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto kupata fursa kuwasilisha malalamiko yao mbele ya UM

Watoto kupata fursa kuwasilisha malalamiko yao mbele ya UM

Itifaki ya ziada kwa mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto imeridhiwa na nchi ya 10 na hivyo kuweka nuru zaidi kwa fursa ya watoto kuwasilisha malalamiko yao ya kunyanyaswa mbele ya kamati ya Umoja wa Mataifa.

Itifaki hiyo ya ziada kwa mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto itaanza kutumika miezi mitatu ijayo ambapo watoto na wawakilishi wao baada ya kuona haki haijatendeka kwenye nchi zao, sasa wataweza kuwasilisha malalamikoyaombele ya kamati ambayo itaamua iwapo uamuzi juu ya suala husika juu ya mtoto lipitiwe upya au la.

Mwenyekiti wa mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto Kirsten Sandberg amesema iwapo malalamiko hayo yakipitiwa na ikibainika kuwepo na makosa, nchi husika itapaswa kuchukua hatua stahili.

Amesema ni hatua ya kihistoria kwani sasa watoto wataweza kusikilizwa kwenye vyombo vya hakikamailivyo kwa watu wazima na ni hatua kubwa katika kusimamia haki za mtoto.

Nchi zilizoridhia itifaki hiyo ya ziada ni Costa Rica, Albania, Bolivia, Gabon, Ujerumani, Montenegro, Ureno, Hispania, Thailand na Slovakia.