Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unatendeka CAR:UM

14 Januari 2014

Ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu yakiwemo mauaji, ukatili wa kimapenzi,watu kukatwakatwa, kutoweka kunyanyaswa, ubakaji na mashambulizi ya kulenga raia makusudi kwa misingi ya kidini umekuwa ukitendeka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati , kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Ripoti ya awali ya timu ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa iliyokuwa nchini humo imeelezea mashambulizi ya kulenga kwa makusudi raia wakiwemo wanawake na watoto yanayofanywa na makundi yanayopinga Balaka na wanamgambo wa zamani wa Seleka.

Ripoti inasema takribani wait 40 wameuwa katika mji mkuu Bangui tangu Ijumaa iliyopita , huku wengine wakitekwa nyara, kukatwakatwa na vitendo vya uporaji.

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay ameonya kuwa licha ya juhudi zinazoendelea za maridhiano , hali ya usalama nchini humo bado ni tete kukiwa na hatari ya mashambulizi zaidi na ukiukwaji wa haki za binadamu. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Baraza la haki za binadamu litakuwa na kikao maalumu Jumatatu ijayo kujadili haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.