WFP yapanua wigo wa usaidizi Sudan Kusini, yalalama kuporwa kwa vifaa

13 Januari 2014

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limezindua operesheni mpya za usaidizi wa kibinadmau kwa waathirika wa mapigano huko Sudan Kusini, huku likishughulikia changamoto zinazokwamisha kufikia wale wanaohitaji misaada zaidi. Grace kaneiya na taarifa kamili

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

 

Kiasi cha dola za Marekani milioni 57.8 kimetengwa ili kufanikisha operesheni hiyo itayodumu kwa muda wa miezi mitatu ambayo itawafikia zaidi ya familia 400,000.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kanda wa WFP Valerie Guarnieri kiasi cha watu 100,000 hadi sasa tayari wamepatiwa misaada mbalimbali tangu mapigano hayo yalipozuka kwa mara ya kwanza katikati ya mwezi Disemba.

Mzozo kwenye eneo hilo umesababisha zaidi ya watu 200,000 kupoteza makazi huku kukiwa na wasiwasi wa idadi hiyo kuongezeka.

WFP inaona kuwa nchi hiyo huenda ikakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa chakula hata kama hali ya kisiasa itatengamaa hapo baadaye.

Kwa upande mwingine mashirika ya utoaji wa misaada ya kiutu yanakabiliwa na wakati mgumu wa kuwafikia raia kutokana na mapigano yanayoendelea