Ban asema hali ya Iraq inamtia hofu, asema jukumu ni la wanasiasa

13 Januari 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa Iraq Nouri Kamel Al-Malik mjini Bagdhad,Iraq hii leo ambapo wameangazia masuala kadhaa ikiwemoSyria, hali nchiniIraqna uhusiano kati ya nchi hiyo naKuwait. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

 (Taarifa ya Assumpta)

Wakati wa mazungumzo hayo Bwana Ban amerejelea tena hofu yake kuhusu hali ya usalama nchiniIraqkufuatia matukio ya hivi karibuni. Wameangazia uchaguzi ujao wa bunge na uhusiano kati ya serikali yaIraqna serikali ya kikanda yaKurdistan. Katibu Mkuu amesema yeye na Waziri Mkuu Al-Maliki wamekubaliana kuwa changamoto zinazokabiliIraqzinahitaji viongozi wa kisiasa kutimiza wajibu wao  kwa kuhakikisha mtangamano wa kijamii, mashauriano na mchakato wa kisiasa wa kuondoa changamoto zilizopo.

Amesema wananchi wa Iraq wanatarajia manufaa na mustakhbali bora kutoka kwa viongozi wao na hivyo uchaguzi ujao wa bunge ni fursa kwa viongozi kutimiza matarajio hayo halali.

 (Sauti ya Ban)

 "Wananchi wa Iraq wanatarajia manufaa kutoka kwa viongozi wao na kwa mustakhabali bora. Uchaguzi ujao wa bunge ni fursa ya kutimiza matarajio hayo halali.”

 Kuhusu Syria ameshukuru Iraq na wananchi wake kwa kufungua mipaka na kusihi jumuiya ya kimataifa kuchangia kwa dhati kwenye mkutano wa kimataifa wa usaidizi wa Syria siku ya Jumatano hukoKuwait. Bwana Ban pia amewasihi viongozi wa Iraq naKuwait kuendeleza azma ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zaokamailivyodhihirika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.