Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kupambana na ukimwi zamulikwa nchini Burundi na Tanzania

Juhudi za kupambana na ukimwi zamulikwa nchini Burundi na Tanzania

Mnamo Alhamisi wiki hii, Kongamano la ngazi ya juu limefanyika huko Washington DC likiangazia vichocheo vya kijamii vinavyoweza kusaidia kutokomeza Ukimwi na umaskini uliokithiri.

Katika kongamanohiloambalo lilijumuisha Benki ya Dunia, Shirika la Mpango wa Maendeleo, UNDP na Shirika linalokabiliana na Ukimwi, UNAIDS, Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS Michel Sidibé alisema kuwa  mabilioni ya dola yanayoelekezwa kwenye sekta hiyo hayawezi kuwa na ufanisi pekee bila kufanyika mabadiliko.

Mabadiliko aliyozungumzia Bwana Sidibé ni pamoja na kubadili fikra ya mshikamano ambao umekuwepo, na kufikiria mshikamano mpya wa kijamii katika kila eneo husika, ili kurejesha usawa na heshima baina ya wanajamii na uwezo wa kutokomeza Ukimwi.