Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na wadau wajizatiti kuwakinga watoto dhidi ya magonwja huko Chad

UNICEF na wadau wajizatiti kuwakinga watoto dhidi ya magonwja huko Chad

Mizozo inayoendelea kwenye maeneo mbali mbali barani Afrika imesababisha wakimbizi kuhama na hivyo kubadili ratiba ya maisha yao ikiwemo kupatiwa chanjo. Huko Chad, wakimbizi kutoka Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati wamejikuta kwenye maeneo tete na kukosa huduma muhimu kama vile chanjo kwa watoto.

Je ni wapi huko na nini kinafanyika kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya msingi ya kuishi kupitia chanjo? Ungana na Assumpta Massoi kwenye ripoti hii.