Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR inasaka taarifa zaidi za ripoti za boti zilizo na wahamiaji kutoruhisiwa kuingia Australia

UNHCR inasaka taarifa zaidi za ripoti za boti zilizo na wahamiaji kutoruhisiwa kuingia Australia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatafuta taarifa zaidi kutoka uongozi wa Australia kuhusu ripoti za karibuni kwenye vyombo vya habari kwamba jeshi la maji wa Australia linazilazimisha boti zinazoshukiwa kubeba waomba hifadhi zinazotaka kuingia nchini humo kurejeaIndonesia.

Pia linafuatilia habari kwamba Australia ina mipango ya kununua na kutoa meli zitakazotumika siku za usoni  kuzifurusha boti hizo zirejee zilikotoka.

UNHCR itatiwa hofu na sera yoyote au vitendo vinavyohusika kufurusha  boti zilizo na wahamiaji kurejea baharini bila kufikiria na kuyachukulia uzito mahitaji ya kila mmoja ya kulindwa.

Limeongeza kuwa mtazamo wowote wa aina hiyo utazusha tafran na uwezekano wa Australia kukiuka wajibu wake chini ya sheria za kimataifa za mkataba wa wakimbizi wajibu wa kisheria wa kimataifa.

Kwa mujibu wa UNHCR kumbukumbu zinaonyesha kuwa vitendokamahivyo ni vigumu kutekeleza na ni za hatari kwa pande zote husika.