Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa amani na maridhiano watoa wito wa amani Sudan Kusini

Viongozi wa amani na maridhiano watoa wito wa amani Sudan Kusini

Viongozi wa makundi ya kikabila wa taasisi za amani na maridhiano kwa pamoja Alhamisi kwa mara ya kwanza wamewataka viongozi wa kisiasa Sudan Kusini kusitisha mapigano mara moja na kuweka mpango wa mani.

Nguzo tatu za kitaifa zinazojumuisha serikali, bunge, jumuiya za kijamii na viongozi wa wanaowakilisha jamii mbalimbali wamewataka wanasiasa kujihusisha katika mchakato wa majadiliano ya kisiasa kama njia pekee ya kutatua mgogoro na kuleta maendeleo kwa wote nchini humo.