Kuharamisha COMANGO Malaysia kunatia wasiwasi:UM

10 Januari 2014

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imesema inatiwa wasiwasi na uamuzi wa karibuni wa wizara ya mambo ya ndani ya Malaysia kutangaza kwamba muungano wa jumuiya 54 za kijamii ujulikanao kama COMANGO nchini humo ni haramu. Taarifa ya Grace Kaneiya Inabainisha zaidi

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Tarehe nane Januari mwaka huu wizara hiyo ilisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba COMANGO ambayo ambayo wanachama wake ni jumuiya zisizo za Kiislam inachagiza haki ambazo haziambatani na Uislam na kwa mujibu wa wizara ni haramu. Wizara pia inasema jumuiya 15 tu kati ya 54 ndio zilizosajiliwa .

COMANGO imedai kwamba imekuwa ikisumbuliwa na kutishiwa na serikali na sekta zisizo za kiserikali. COMANGO imekuwa ikishutumiwa kushambulia Uislamu na kusambaza imani zinazokiuka mafunzo ya Uislam.

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa na mkuu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa Navi Pillay kila mara imetoa wito wa kuwalinda watu na makundi dhidi ya vitisho au ulipizaji kisasi. Rupert Colville anaeleza zaidi

 “Muungano huo umeshtumiwa kwamba una lenga dini ya kislamu na kwamba mafunzo yake yanakiuka maadili ya ya Kislamu, tunahofu kuhusu vitendo vya kujilipiza kisasi dhidi ya COMANGO kwa sababu ya ushirikiano wao na mashirika ya kimatiafa ya haki za binadamu. Tunaitolea wito serikali ya Malaysia kurekebisha  sheria yake ya mwaka  1966, kuimarisha mazingira kuwezesha mashirika ya haki za bindamu kutekeleza shughuli zake bila kujali kukandamizwa au unyanyasaji.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter