Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mali ina fursa ya kujikwamua kiuchumi baada ya mzozo: IMF

Mali ina fursa ya kujikwamua kiuchumi baada ya mzozo: IMF

Shirika la Fedha duniani, IMF limesema Mali baada ya mapigano inaweza kuibuka na kujikwamua kiuchumi iwapo tu itaweza kutambua na kufungua fursa ilizonazo. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Kidole kimoja hakiokoti  jiwe, methali maarufu nchiniMali ambayo Mkurugtenzi Mtendaji wa IMF Christine Lagarde aliitumia kuhitimisha hotuba yake mbele ya wajumbe wa baraza la kiuchumi na kijamii mjini Bamako hii leo. Amesema kama vidole vyote vinavyotakiwa kutumika kuokota jiwe, ndivyo Mali inavyotakiwa kujumuisha jamii zote na watu wote, vijana, wanawake na wanaume bila kujadili jinsia, imani za kidini katika kujikwamua kiuchumi.

Amesema fursa zipo na kinachohitajika ni sera thabiti na ubia wa sekta binafsi na umma ili kuendeleza mwelekeo mzuri wa kiuchumi, kisiasa na kijamii uliokuwepo kabla ya mzozo.

Bi. Lagarde amesema barani AfrikaMaliilikuwa ni mojawapo ya nchi zilizoelekea kutimiza malengo ya milenia na kwamba maendeleo ya kisiasa yaliyotokea hivi karibuni ni dalili kuwa raia waMalini wavumilivu na jasiri katika kusongesha mbele nchiyaona IMF iko tayari kuunga mkono jitihada hizo.