Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yasaka dola milioni 99 kwa ajili ya Sudan Kusini na CAR

UNHCR yasaka dola milioni 99 kwa ajili ya Sudan Kusini na CAR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa ombi la dola milioni 99 ili kuwasaidia maelfu ya watu waliotawanywa na machafuko na hali mbaya Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.

Fedha hizo ni kwa ajili ya watu wa Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati waliofungasha virago na kuzikimbia nchi zao pamoja na wakimbizi wa ndani.

Dola hizo milioni 99 zitagawanywa kwa mataifa hayo mawili , Sudan Kusini dola milioni 59 na CAR dola milioni 40.2 kwa kipindi cha kuanzia sasa hadi Machi.

Ombi la leo linadhihirisha hali ni mbaya kiasi gani kwa mataifa hayo mawili ambako maelfu kwa maelfu  ya watu wameathirika.