Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka mataifa kuchangia fedha za kuinusuru Syria

Ban ataka mataifa kuchangia fedha za kuinusuru Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitaka nchi wanachama wa umoja huo kuhudhuria katika kongamano la pili la kutoa ahadi za ufadhili kwa ajili ya misaada ya kiutu kwa ajili ya mahitaji ya kibinadamu na kuimarisha Syria na nchi jirani zake, ikiwemo Lebanon.

Akiongea mjini New York msemaji wa Katibu Mkuu Farhan Haq amesema Bwana Ban ambaye anatarajiwa kusafiri wiki ijayo kuongoza kongamano hilo mnamo January 15 ambalo limeandaliwa na Mfalme wa Kuwait, Sheikh Sabah Al Ahmed Al Jaber Al Sabah, anatarajiwa pia kukutana na viongzoi wa ngazi za juu wa taifa hilo pamoja na viongozi wengine wanaohudhuria mkutano huo.

Amesema Katibu Mkuu amezitaka nchi wanachama kujitolea kusaidia Syria ambayo hali yake ya kibinadamu inazidi kuzorota.

 Mzozo wa Syria umesababisha mzigo kwa mataifa jirani mathalani Lebanon ambayo inahifadhi wakimbizi 860,000 na ambayo kwa mujibu wa Mratibu Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Derek Plumbly inahitaji dola bilioni 1.7