Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Plumbly akutana na Waziri wa Kuwait kabla ya kongamano la wafadhili

Plumbly akutana na Waziri wa Kuwait kabla ya kongamano la wafadhili

Mratibu Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, Derek Plumbly, amekutana leo na Waziri Mtendaji wa Masuala ya Kijamii wa Kuwait, Wael Abou Faour kujadili maandalizi ya kongamano la wafadhili nchini humo, ambalo limepangwa kufanyika mnamo tarehe 15 Januari. Kongamano hilo la kutoa ahadi za ufadhili limeandaliwa na Mfalme wa Kuwait, Sheikh Sabah Al Ahmed Al Jaber Al Sabah, na litasimamiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Lengo la kongamano hilo ni kumulika athari za hali ya kibinadamu inayoendelea kuzorota, na kuchagiza uchangiaji fedha kwa ajili ya mahitaji ya kibinadamu na kuimarisha Syria na nchi jirani zake, ikiwemo Lebanon.

Bwana Plumbly amesema kuwa Lebanon, ambayo itahitaji dola bilioni 1.7 kutokana na kongamano hilo, imeathirika kwa kiasi kikubwa mno na mgogoro wa Syria, ikiwa sasa inawapa hifadhi wakimbizi 860,000 walosajiliwa, ambayo ndiyo idadi kubwa zaidi katika nchi yoyote ile kwenye ukanda mzima. Ameipongeza Lebanon kwa ukarimu wake, na kwa kuendelea kufungua mipaka yake.