Familia zilizopoteza makazi Syria zaonana na mkuu wa WFP

9 Januari 2014

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP Ertharin Cousin amehitimisha ziara yake ya siku moja nchini Syria iliyomkutanisha na viongozi wa ngazi za juu serikalini na familia zilizopo mji mkuu Damascus baada ya kupoteza makazi  yao kutokana na mapigano.

Familia hizo ni zile zinazopata mgao wa chakula mjini humo ambapo Bi. Cousin amesema hali ya kibinadamu nchiniSyriainazidi kuwa ngumu kila uchao wakati huu ambapo nusu ya wasyria hawana uhakika wa chakula.

Akiwa kwenye kituo cha mgao wakati wa ziara hiyo ya siku moja, aliweza kuzungumza na wanawake ambapo mmoja wao alimweleza kuwa amekuwa akibadilisha makazi ya muda baada ya nyumba hao kuharibiwa. Amemweleza kuwa tegemeo lao sasa ni WFP kwani hakuna yeyote kwenye familiayaoaliyeweza kupata ajira.

Bi, Cousin amesema licha ya kuongeza msaada wa chakula mwezi huu ili kufikia zaidi ya watu Milioni Nne, bado changamoto ni kufika maeneo ambako kuna mapigano. Mkuu  huyo wa WFP amesema bila kuwafikia watu hao, azmayaoya kuongeza usaidizi haiwezi kufikiwa.

Amesema janga laSyriani zaidi ya kupata idadi ya watu kwani kifikra watu wameathirika zaidi kutokana na kupoteza jamaa zao. Amesema ni muhimu jamii ya kimataifa kuendeleza usaidizi wa kibinadamu.