Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IPU yakaribisha makubaliano ya kisiasa kuhusu ulinzi wa wabunge wa Uturuki

IPU yakaribisha makubaliano ya kisiasa kuhusu ulinzi wa wabunge wa Uturuki

Muungano wa Kimatatifa wa Wabunge, IPU, umekaribisha makubaliano yalofikiwa wiki hii na vyama vitatu vya kisiasa nchini Uturuki ya kufanyia marekebisho katiba ya kitaifa ili iweke wazi ni katika mazingira yepi afisa aliyechaguliwa anaweza kushtakiwa au kufungwa.

Makubaliano hayo yanatazamia kupanua uwanja wa ulinzi wa wabunge na kutatua tatizo la wabunge kadhaa waliofungwa, kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa IPU, Anders B. Johnsson.

IPU inaamini kuwa kuweka tume ya mseto wa vyama ili itekeleze marekebisho ya katiba ni hatua muhimu ambayo itawaruhusu wabunge kutekeleza haki yao kuwawakilisha watu walowachagua.