Vichocheo vya kijamii ni muhimu kujumuishwa ili kuondokana na Ukimwi na Umaskini

9 Januari 2014

Kongamano la ngazi ya juu linafanyika huko Washington DC, nchini Marekani likiangazia vichocheo vya kijamii vinavyoweza kusaidia kutokomeza Ukimwi na umaskini uliokithiri. Ripoti ya Joshua Mmali  inafafanua zaidi.

(Ripoti ya Joshua)

Wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo Benki ya Dunia, shirika la mpango wa maendeleo-UNDP na lile linalokabiliana na Ukimwi, UNAIDS walitoa mada za uchokozi kwenye kongamano hilo. Mtendaji Mkuu wa UNAIDS, Michel Sidibé akaweka bayana kuwa mabilioni ya dola yanayoelekezwa kwenye sekta hiyo hayawezi kuwa na ufanisi pekee bila kufanyika mabadiliko..

(Sauti ya Sidibe)

“Utaweka mabilioni ya dola, lakini hautawaondoa watu kwenye umaskini uliokithiri!Unatakiwa kubadili kabisa fikra ya mshikamano ambayo imekuwepo. Sintofahamu tuliyo nayo sasa ya kutokuwepo heshima hata kwa uhai wa mtu! Kwenye maeneo hayo mengi ni lazima sisi kushughulikia jambo hilo.”

Bwana Sidibé amesema ni lazima kufikiria aina mpya ya mshikamano wa kijamii katika kila eneo husika, mshikamano ambao amesema utarejesha usawa baina ya wanajamii na hata kuheshimiana na hata kutokomeza Ukimwi na umaskini uliokithiri.