Uganda yatathmini ardhi inayozozaniwa na wananchi na wakimbizi

9 Januari 2014

Nchini Uganda kazi imeanza ya kufungua mpaka wa ardhi inayozozaniwa kati ya wakimbizi wanaoishi kambi ya Kyangwali na wananchi wa eneo hilo. Miongoni mwa wakimbizi hao ni wale wanaotoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kama anavyoripoti John Kibego wa redio washirika ya Spice FM, Uganda.

(Tarifa ya John Kibego)

Ufurushwaji wa zaidi ya watu elfu hamsini waliodaiwa kuvamia ardhi ya kambi hiyo yenye ukubwa wa miali 51 nraba, ulianza mwaka ulipita na kusitishwa wiki chache baadaye kwa misingi kwamba ungeliheiki kuwa janga la kibinaadamu.

Wizara ya kushugulikia majanga iliagiza mipaka ya ardhi hiyo ifunguliwe ili kubaini mvamizi na yule aisyekuwa mvamizi kabla ya kuwafurusha. Sasa, masoroveya wameanza kazi ya kufungwa mipaka huko usajili wa waliopo kwenye ardhi hiyo ukiendelea.

Meja Jenerali Julius Oketta, Mkurugenzi wa kitaifa wa uratibu wa madharura, ndiye mwenye kiti wa kamati ya zoezi hili.

(Sauti ya Mej. Gen. Julius Oketta)

Uhitaji wa kufurusha wavamizi wa ardhi ya kambi ya wakimbizi ulitokea kufuatia kumiminika kwa wakimbizi kutoka nchi jirani ya Jamhuri ua Kidemokrasia ya Congo, (DRC).