Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wahaha kuwanusuru wakimbizi nchini Iraq.

UM wahaha kuwanusuru wakimbizi nchini Iraq.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Nickolay Mladenov amesema umoja huo unafanya kazi kwa karibu na mamlaka za kitaifa na kikanda nchini Iraq pamoja na washirika wa misaada ya kiutu kuhakikisha misaada ya kiutu na ya dharura inawafikia salama watu waliokwama pamoja na familia zilizopoteza makazi katika jimbo liitwalo Anbar.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Bwana Mladenov amesema hali ya kiutu ni mbaya huko Anbar wakati huu ambapo operesheni zinaendelea. Amesema mashirika ya Umoja wa Mataifa yanafanya kazi ya kuainisha mahitaji ya watu na kuandaa misaada ya dawa, chakula na misaada mingine isiyo ya vyakula tayari kwa ajili ya kuwafikia walengwa ikiwa usalama utahakikishwa.

Kadhalika mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu ameelezea kusikitishwa kwake na hali eneo liitwalo Fallujah ambako akiba ya chakula, maji na dawa za kunusuru maisha zinaelezwa kuisha.

Tathimini ya awali inaonyesha kuwa zaidi ya familia 5,000 zimekimbia mapigano ma kutafuta ifadhi katika majimbo jirani na kwingineko. Umoja wa Mataifa unafanya kazi na wizara inayohusika na watu walipoteza makazi na na uhamiajinchini Iraq ili kuuainisha mahitaji ya raia hao na kuwafikia haraka.