Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada ya haraka yahitajika CAR kunusuru wakimbizi :UM

Misaada ya haraka yahitajika CAR kunusuru wakimbizi :UM

Jumuiya ya kimataifa imetakiwa kutoa kwa haraka raslimali toshelevu kwa ajili ya kulinda na kusaidia mahitaji ya idadi kubwa na inayokuwa ya watu waliopoteza makazi kufuatia ghasia katika jamahuri ya Afrika ya Kati, CAR. Amesema mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za watu waliopoteza makazi Chaloka Beyani.

Katika taarifa yake Bwana Beyani amesema idadi ya watu waliopoteza makazi imeongezeka kwa kasi katika wiki chache  zilizopita na kusema kuwa lazima vikwazo vya kuwafikia waathirika  viondolewe haraka ili kuwezesha mashirika ya misaada ya kiutu kuwafikia walengwa wakiwemo wakimbizi wanaojihifadhi katika uwanja wa ndege waBanguibila kuchelewa.