Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaanza tena kuwalisha wakimbizi wa ndani CAR

WFP yaanza tena kuwalisha wakimbizi wa ndani CAR

Shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeanza tena kugawa chakula kwa familia za wakimbizi wa ndani kwenye uwanja wa ndege wa Bangui nchini Jamhuri ya Afrijka ya kati ambako inasemekana watu wapatao 100,000 wamepata hifadhi. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Ugawaji huo umeanza tena baada ya kusitishwa kwa wiki tatu kutokana na hali ya usalama kwenye enao hilo. Ugawaji huo ulianza Jumanne jioni bila tukio lolote na unaendelea leo Jumatano

Katika siku ya kwanza ya ugawaji chakula milo ilitolewa kwa watu 5,490, na WFP na washirika wake wana mpango wa kugawa chakula hicho kwa muda wa siku 10 kwa wakimbiozi wa ndani wote walioko kwenye uwanja wa ndege wa Bangui.

WFP inashirikiana na shirika la wakimbizi UNHCR, la watoto UNICEF na ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA , NGO ya Italia COOPI na viongozi wa kijamii kwa wiki chache zilizopita iki kuhakikisha mazingira yanaruhusu kusambaza msaada wa chakula na misaada mingine kwa wakimbizi wa ndani.

WFP imeshukuru vikosi vya Ufaransa, na askari wa Muungano wa Afrika misca kwa kuhakikisha usalama wakati wa ugawaji chakula.