Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yahofia matumizi ya nguvu kupita kiasi Cambodia

Ofisi ya haki za binadamu yahofia matumizi ya nguvu kupita kiasi Cambodia

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Navi Pillay amesema anafuatilia kwa karibu na kwa hofu hali nchiniCambodiaya matumizi ya nguvu kupita kiasi inayofanywa na vikosi vya usalama kukabili waandamanaji. Joshua Mmali na maelezo zaidi

 (TAARIFA YA JOSHUA MMALI)

Kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu Ijumaa ya tarehe 3 Januari watu watano waliuawa wakati vikosi vya usalama vilipofyatua risasi kwenye kundi la waandamanaji .

watu wengine 20 walijeruhiwa kwa risasi na kipigo. Pillay ameutaka uongozi waCambodiakuanzisha uchunguzi wa haraka na wa kina na kuhakikisha wahusika wa matumizi ya nguvu kupita kiasi wanawajibishwa. 

Pia ameitaka serikali ya nchi hiyo kuhakikisha viwango vya kimataifa katika matumizi ya nguvu vinazingatiwa.,kamaanavyofafanua msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Rupert Colville

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Tunaitolea wito serikali yaCambodiana vikosi vya usalama kujizuia na matumizi ya nguvu. Kufuatilia waandamanaji lazima kuzingatie wajibu wa kimataifa wa haki za binadamu na viwango vya kimataifa vya kuhakikisha kuna utulivu wa umma.”

Watu wengine 23 na mtoto mmoja bado hawajulikani waliko, walikamatwa Ijumaa na Umoja wa Mataifa unataka mahabusu wote wapewe fursa za uwakilishi wa kisheria.