Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya iko katika mwelekeo sahihi kuimarika kiuchumi: IMF

Kenya iko katika mwelekeo sahihi kuimarika kiuchumi: IMF

Kenya iko kwenye mwelekeo sahihi wa kuimarika kiuchumi na kiniachotakiwa ni kutekeleza mambo makuu matatu ili isiende mrama, amesema Mkurugenzi mtendaji wa shirika la fedha duniani, IMF Christine Lagarde wakati wa kongamano la sekta binafsi mjini Nairobi.

Bi Lagarde ametoa mfano wa vile ambavyo Kenya imeweka mazingira yanayojumuisha wananchi katika mfumo wa fedha ili waweze kupata mikopo na kushiriki kwenye sekta za kiuchumi na kuinua maisha yao.

Ametaja mazingira hayo kuwa ni pamoja na sera sahihi za fedha zinazodhibiti deni la ndani na la nje na usimamizi thabiti unaohakikisha utulivu katika uchumi.

Kutokana na hali hiyo Bi. Lagarde amesema Kenyai mejiweka katika nafasi bora ya kuvutia vitega uchumi vya kimataifa. Hata hivyo amesema ili mwelekeo sahihi wa uchumi uweze kuimarika zaidi Kenya inapaswa kugatua mfumo wa fedha, kuondoa tofauti ya matumizi ya rasilimali na kuendeleza ushirikiano wa kikanda.